CAR-UFARANSA-SANGARIS

Askari 6 wa Ufaransa waondolewa mashtaka ya ubakaji CAR

Askari wa kikosi cha Ufaransa Sangaris wakipiga doria pembezoni mwa mji wa Boda, kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya kati, Julai 24 mwaka 2014.
Askari wa kikosi cha Ufaransa Sangaris wakipiga doria pembezoni mwa mji wa Boda, kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya kati, Julai 24 mwaka 2014. AFP PHOTO / ANDONI LUBAKI

Mahakama nchini Ufaransa, imewaondolea mashtaka wanajeshi sita ambao wamekuwa wakishtumiwa kuwabaka wasichana wenye umri mdogo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu wa Mahakama unamaanisha kuwa wanajeshi hao hawatafunguliwa mashtaka kama ilivyokuwa imetarajiwa baada ya kuzuka kwa tuhma hizi.

Tuhma hizi, ziliwakuumba wanajeshi wa Ufaransa waliokuwa wamekwenda kulinda amani nchini humo mwaka 2013 baada ya mapinduzi dhidi ya rais François Bozize.

Ripoti kutoka idara ya Mahakama nchini Ufaransa, zinasema kuwa baada ya uchunguzi wa kutosha, imebainika kuwa hakuna ushahidi wowote wa kuwafungulia mashtaka wanajeshi hao.

Hii inamaanisha kuwa, tuhma dhidi ya wanajeshi hawa zitafutwa lakini walalamishi wana miezi mitatu kudai uchunguzi mpya dhidi ya wanajeshi hao wa Ufaransa.