UNGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Theresa may atangaza hadharani kuvunjika kwa uhusiano na EU

Theresa May akiondoka katika Lancaster House, ambapo alitoa hotuba kuhusu kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya , Januari 17, 2017.
Theresa May akiondoka katika Lancaster House, ambapo alitoa hotuba kuhusu kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya , Januari 17, 2017. REUTERS/Leon Neal

Katika hotuba aliotoa Jumanne Januari 17 mjini London, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May alitetea kuvunjika kwa wazi kwa ushirikiano na Umoja wa Ulaya, na kusema kuwa kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya pia kulimaanisha kuondolewa kwa soko la pamoja.

Matangazo ya kibiashara

Theresa May anataka kufikiwa na Umoja wa Ulaya mkataba wa ushirikiano wa kudumu ndani ya miaka miwili ijayo. Mkataba huu utatekelezwa kwa hatua ili kuepuka kujiondoa ghafla. Lakini hakuna suala la kukaa mguu mmoja ndani, mguu mmoja nje.

Waziri Mkuu wa Uingereza pia ametangaza kuondolewa kwa soko la pamoja na Mahakama ya Ulaya, kwa sababu kipaumbele cha nchi yake ni kurejesha udhibiti wa mipaka yake. Badala yake, Waziri Mkuu anataka kupata "haki ya moja kwa moja katika soko la Umoja wa Ulaya" na anapendelea kusainiwa kwa mkataba wa biashara huria "kabambe na wenye kina" na Brussels, wakati ambapo 49% ya mauzo ya nje ya Uingereza yalikwenda barani Ulaya mwaka 2016.

Baadhi wamepinga madai hayo ya Theresa May kama Waziri Mkuu wa zamani wa Sweden Carl Bildt ambaye amekata tamaa. Anaamini kwamba Theresa Mei achagua mfano ambao umoja wa Ulaya ungelikua na uhusiano zaidi na Ukraine kuliko Uingereza. Katika ujumbe uliorushwa kwenye akaunti yake ya Twitter, rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk, amesema hotuba ya Theresa May imejaa "ukweli" kuliko awali. "Mchakato wa kusikitishwa, kwa wakati usiofaa, lakini angalau tangazo hilo limejaa ukweli kuhusu kujiondoa kwa Ungereza katika Umoja wa Ulaya," alijibu Bw Tusk, huku akihakikisha kwamba Umoja wa Ulaya ikiwa na wanachama 27 ilikuwa na "umoja na ilikua tayari kujadili" kama Ibara ya 50 ingelizua utata.