MARKANI-UINGEREZA-USHIRIKIANO

Waziri Mkuu wa Uingereza kukutana kwa mazungumzo na Trump

Theresa May akutana kwa mazungumzo na Donald Trump.
Theresa May akutana kwa mazungumzo na Donald Trump. REUTERS/Dylan Martinez

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May anatarajiwa kukutana na rais wa Marekani Donald Trump, kujadiliana kuhusu maswala mbalimbali yanayokumba nchi hizo mbili na dunia.

Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kukutana na rais Trump, Waziri Mkuu May amesema Uingereza itaendeleza urafiki wake wa karibu na Marekani, lakini amemuonya Trump kuwa karibu sana na Urusi, lakini pia kuendelea kusaidia katika vita dhidi ya ugaidi.

Theresa May anakuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana na rais Trump.

Akizungumza mjini Philadelphia, ikiwa ni mwanzo wa ziara yake nchini MarekaniBi May amesema kwa uhakika nchi yake ambayo imemaliza uanachama wake kwenye Umoja wa Ulaya, iko tayari kujenga ushirikiano na marafiki zake wa zamani na wapya pia.