UFARANSA-UGAIDI-IS-IRAQ

Mmoja wa wanajihadi wa Ufaransa aliokua akitafutwa auawa

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na LCI Ijumaa usiku, mmoja wa watu muhimu wa kundi la IS aliyekua akiajiri wapiganaji katika kundi hilo inasadikiwa kuwa aliuawa Jumatano, Februari 8 na mashambulizi ya angani ya muungano wa kimataifa. Lakini serikali ya Ufaransa bado inasubiri uthibitisho wa taarifa hii.

Mpiganaji wa Dola la Kiislam akishikilia bendera nyeusi ya Islamic State, karibu na mpaka wa Iraq na Syria.
Mpiganaji wa Dola la Kiislam akishikilia bendera nyeusi ya Islamic State, karibu na mpaka wa Iraq na Syria. ALBARAKA NEWS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Ufaransa badoinasubiri uthibitisho wa mwisho wa kifo chake. katika mitandao ya kijamii ya wanajihadi na Telegram, kuna ujumbe uliorushwa hewani unaotolea wito wa kuwamuombea Rashid Kassim.

Inasadikiwa Rashid Kassim aliuawa siku mbili silizopita na mashambulizi ya angani ya muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani katika mkoa wa Mosul, nchini Iraq.

Rashid Kassim, mwenye umri wa miaka 29 alikua kwa muda mrefu akitafutwa na Ufaransa pamoja na Marekani. Alikua mmoja wa magaidi wa Ufaransa aliyekua akitafutwa duniani. Jina lake linaonekana karibu kwenye mipango yote ya mashambulizi, mashambulizi yote ya kigaidi yaliofanyika katika ardhi ya Ufaransa tangu majira ya joto mwaka jana.

Rashid Kassim alijulikana kwa kuonekana mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii. alikua akirusha video zenye lengo la kuchochea ugaidi, na alikua akiandika ujumbe wa kutolea wito wanajihadi kufanya mashambulizi.