Afisa wa zamani wa CIA aachiwa huru Ureno

Afisa wa zamani wa CIA, Sabrina de Sousa (kulia). Tarehe 1 Machi 2017.
Afisa wa zamani wa CIA, Sabrina de Sousa (kulia). Tarehe 1 Machi 2017. REUTERS/Pedro Nunes

Afisa wa zamani shirika la kijasusi la Marekani (CIA), Sabrina de Sousa, ambaye alihukumiwa mwaka 2009 hadi miaka minne jela nchini Italia kwa kosa la kumteka nyara mwanadini wa Misri mwaka 2003, alipata Jumatano katika dakika za mwisho taarifa kutoka Ureno kwamba hatosafirishwa Italia na kwamba ameachiwa huru, wakili wake ametangaza.

Matangazo ya kibiashara

Afisa huyo wa zamani wa CIA, aliyekamatwa wiki iliyopita nchini Ureno, alikuwa tayari kwenye uwanja wa ndege wa Lisbon akielekea Italia wakati taarifa ya kukamatwa kwake ilipowasilishwa na pilisi ya Interpol, alisema wakili wake, Manuel Magalhaes e Silva.

"Mwendesha mashitaka wa mahakam ya Milan imebadilisha uamuzi wa kumuweka kizuizini. Polisi ya Interpol wa Italia ambao wako hapa kwa kumsafirisha wamepewa taarifa hiyo na hatosafirishwa tena," mwanasheria wake ameongeza.

Sabrina de Sousa, ambaye ni Mmarekani mwenye asili ya Ureno, baadaye aliachiwa huru.

"Kwa sasa Sabrina yuko huru. Tunakisubiri uamuzi wa mahakama ya Italia kuhusu adhabu mbadala gerezani, " amebaini wakili manuel magalhaes e Silva.

Rais wa Italia Sergio Mattarella, Jumanne wiki hii alitoa msamaha kwa Sabrina de Sousa, na hivo kupunguza adhabu yake kifungo kutoka miaka minne hadi mitatu.

De Sousa ni sehemu ya kundi la watu 26 waliohukumiwa kwa kuhusika katika utekaji nyara wa kiongozi wa kidini, Sheikh Osama Moustafa Hassan Nasser, mwaka 2003.