UFARANSA-UCHAGUZI 2017

Viongozi wa Le Republicane nchini Ufaransa wataka mgombea mwingine

François Fillon ameendelea kupoteza uungwaji mkono nchini Ufaransa
François Fillon ameendelea kupoteza uungwaji mkono nchini Ufaransa REUTERS/Jean-Paul Pelissier

Mgombea urais nchini Ufaransa Francois Fillon anakabiliwa na wakati mgumu kufuatia kashfa iliyomkumba katika harakati za kampeni wakati mkongwe wa kihafidhina Alain Juppe akijiweka tayari kuchukua nafasi yake katika mbio za kuelekea ikulu.

Matangazo ya kibiashara

Tayari Msemaji na meneja wa kampeni za Fillon amejiengua na kiongozi wa chama hicho kidogo cha mrengo wa kati amethibitisha kuwa hataendelea kuunga mkono kashfa kubwa inayomkabili Fillon.

Shinikizo limeelekezwa kwa waziri mkuu wa zamani kutoka mrengo wa kulia ambaye anatimiza umri wa miaka 63 leo jumamosi, tangu mahakama kuagiza uchunguzi kufanyika dhidi yake kuhusu madai ya kutoa malipo kwa mkewe kwa kazi ambayo hakuifanya.

Kujiuzulu kwa Thierry Solère ni mfululizo wa viongozi wa ndani ya chama hicho waliotangaza kujiondoa kwenye kampeni za Fillon baada ya kuibuka kwa tuhuma za ubadhirifu dhidi yake.

Solère, ambaye alimuunga mkono Bruno Le Maire, wakati wa kura za awali za maoni amesema haileti maana yoyote kuendelea kuwa kwenye kampeni za mgombea ambaye anakabiliwa na kashfa kubwa kama hii.

Katika mfululizo wa kudumaza kampeni zake, mhasibu wa kampeni za Fillon, Gilles Boyer, kaimu meneja wake wa kampeni Sebastiba Lecorn na mwakilishi wake wa masuala ya kimataifa, Bruno Le Maire wote kwa pamoja wametangaza kujiondoa kwenye kampeni za Fillon juma hili.