UFIKIPINO-UJERUMANI-UGAIDI

Mwili wa mateka aliyekatwa kichwa Ufilipino wapatikana

Jurgen Kantner na mkewe Sabine Merz (kulia). Picha iliyopigwa Mei 5, 2009 katika mji wa Berbera.
Jurgen Kantner na mkewe Sabine Merz (kulia). Picha iliyopigwa Mei 5, 2009 katika mji wa Berbera. AFP/Mustafa ABDI

Mwili wa mateka kutoka Ujerumani ambaye alikatwa kichwa na wanamgambo wa kiislamu nchini Ufilipino wiki hii umepatikana baada ya kutafutwa kwa siku kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

Jurgen Kantner alitekwa nyara kutoka kwa mashua yake ya kifahari mwezi Novemba. Wakati huo huo kundi la wanamgambo wa Abu Sayyaf linasema kuwa ndilo lilihusika na kisa hicho.

Mwili wake ulipatikana katika kisiwa cha Sulu na utarudishwa nchini Ujerumani.

Na mwili wa mkewe Kantner, Sabine Merz ulipatikana ukiwa na jeraha la risasi ndani ya mashua hiyo iliyokuwa imetelekezwa mwezi Novemba

Abu Sayyaf ni moja ya makundi madogo zaidi lenye ghasia mbaya kusini mwa Ufilipino, kutokana na dhuluma zake ikiwemo ukataji vichwa.

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte mapema aliomba msamaha kwa familia ya Kantner na kwa viongozi wa Ujerumani, kwa kushidwa kumuokoa kwa karibu miezi minne baada ya kusisitiza kuwa fidia haitalipwa.

Wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Ujerumani ilisema kuwa imepata mshutuko mkubwa kufuatia kitendo hicho cha kinyama.