UJERUMANI

Ujerumani: Polisi yasema aliyejeruhi abiria kwa shoka alikuwa na matatizo ya akili

Polisi wakilinda stesheni ambayo mtu mwenye shoka alikuwa akishambulia abiria nchini Ujerumani.
Polisi wakilinda stesheni ambayo mtu mwenye shoka alikuwa akishambulia abiria nchini Ujerumani. REUTERS/Petra Wischgoll

Polisi wa Ujerumani wanasema kuwa mtu mmoja aliyewajeruhi watu zaidi ya 9 usiku wa kuamkia leo kwenye kituo kimoja cha Treni, alikuwa na matatizo ya akili, taarifa inayokanusha kuwa lilikuwa ni tukio la kigaidi.

Matangazo ya kibiashara

Polisi wanasubiri hivi sasa kumuhoji mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 36 aliyetokea Kosovo na kwa sasa anapatiwa matibabu hospitalini baada ya kudakwa akijaribu kuruka kwenye daraja kuwakimbia polisi.

Mtuhumiwa huyo ametambulika kwa jina moja tu la Fatmir, ambaye baada ya kukamatwa aliwaambia maofisa wa polisi kuwa alitarajia kuona polisi wakimlen

The suspect sparked panic when he got off a commuter train late Thursday and began swinging an axe at passers-by. Police said he was in an "exceptional mental state" at the time.

Makomandoo wa polisi waliovalia vifaa maalumu, walifika kwenye stesheni hiyo wakisaidiwa na helcopta, kwa kile ambacho awali kilielezwa kuwa huenda lilikuwa ni shambulio la kigaidi.

Kukiwa na michirizi mingi ya damu baada ya watu kujeruhiwa, polisi walianza kumfukuza mtuhumiwa wa shambulio lenyewe hadi pale walipomkamata kwenye daraja ambalo alikuwa akijaribu kutoroka.

Msemaji wa jeshi la Polisi nchini Ujerumani, amesema kuwa maofisa wameondoa uwezekano wa kuwa lilikuwa shambulio la kigaidi na kwamba mtuhumiwa alitoka kwenye mji wa Wuppertal ulioko umbali wa kilometa 30 na mji wa Duesseldorf ambako alitekeleza shambulio.

Nchi ya Ujerumani imeendelea kushuhudia matukio ya aina hii katika kipindi cha miezi minne iliyopita, huku kati yao yakitekelezwa na watu walio na matatizo ya akili, lakini shambulio la mwezi Desemba mwaka jana ambapo mtuhumiwa alitumia lori la mizigo, lilidaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State.