UFARANSA-FILLON-SIASA-HAKI

François Fillon kuchunguzwa

Mgombea wa chama cha RepublicanFrançois Fillon katika mkutano mjini Besançon (Doubs), Alhamisi, Machi 9, 2017.
Mgombea wa chama cha RepublicanFrançois Fillon katika mkutano mjini Besançon (Doubs), Alhamisi, Machi 9, 2017. Sébastien BOZON / AFP

François Fillon anachunguzwa na mahakama ya mjini Paris, nchini Ufaransa katika kesi ya ajira hewa baada ya kushtumiwa kuwalipa mishahara watu wa familia yake.

Matangazo ya kibiashara

Mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa urais alionekana Jumanne wiki hii mbele ya jaji anayehusika na kesi hiyo.

François Fillon anakanusha mashtaka yanayomkabili.

Bw Fillon, waziri mkuu wa zamani anashitakiwa kwa kosa la ubadhirifu wa mali ya umaa, ufichuzi na kula njama za matumizi mabaya ya mali ya jamii.

Ofisi ya mashitaka pia inamtuhumuwa kosa la kutowajibika kutangaza kwenye Mamlaka kuu matumizi ya mali ya umma

Fillon, bado mgombea

François Fillon alikubali mwezi uliopita, kuwa alifanya "kosa" kwa kuajiri mke na watoto wake kwa kazi ya usaidizi katika Bunge.

Aliomba "msamaha" kwa wananchi wa Ufaransa akisisitiza kuwa atawania katika uchaguzi wa urais.