UTURUKI-EU-MVUTANO

Uturuki yasitisha uhusiano wa kidiplomasia na Uholanzi

Ankara inaona kuwa hatua ya polisi kuingilia dhidi ya mkutano wahadhara wa  raia wake waishio ugenini Jumamosi usiku Machi 11 mbele ya ubalozi mdogo wa Uturuki katika mji wa Rotterdam ni kinyume na sheria.
Ankara inaona kuwa hatua ya polisi kuingilia dhidi ya mkutano wahadhara wa raia wake waishio ugenini Jumamosi usiku Machi 11 mbele ya ubalozi mdogo wa Uturuki katika mji wa Rotterdam ni kinyume na sheria. REUTERS/Yves Herman

Uturuki imeghabishwa na hatuwa ya nchi za Ulaya kuwazuia mawaziri wake kuendesha mikutano ya hadhara katika mataifa ya Ulaya na sasa imemzuia balozi wa Uholanzi jijini Ankara kuondoka nchini humo huku ikimtuhumu kansela wa Ujarumani Angela Merkel kuunga mkono ugaidi.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuyaita mataifa ya Ulaya kuwa ya kinazi, serikali ya Ankara imetangaza kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Uholanzi na kumzuia balozi wake Kees Cornelis van Rij hadi pale masharti yaliotolewa yatapotekelezwa.

Miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kufanya uchunguzi kuhusu matukio ya hivi majuzi ambapo polisi wa Uholanzi walitumia farasi na mmbwa katika kuwatawanya waandamanaji raia wa Uturuki waliokuwa wakiandamana katika Ubalozi mdogo wa Uturuki jijini Rotterdam.

Mkuu wa sera za mambo ya nje kwenye Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amesema ni vema kutatua mzozo huo haraka iwezekanavyo ili kupunguza joto hilo kuendelea kupanda zaidi, wakati huo huo Marekani imezitaka pande zote mbili kutatua mzozo huo wa kidiplomasia.

Mvutano huo umeibuka tangu juma lililopita ambapo Ujerumani ilimzuia waziri wa mambo ya nnje wa Uturuki kuwahutubia raia wa uturuki waliopo nchini humo kwa ajili ya kampeni za uchaguzi was kura ya maoni inayotarajiwa kupigwa hivi karibuni nchini Uturuki.

Tukio ambalo liliripotiwa pia nchini Uholanzi na kuzua ghadhabu kwa viongozi wa Uturuki.