UTURUKI-EU-MVUTANO

Erdogan aishutumu EU kuanzisha kampeni ya kupinga Uislamu

Recep Tayyip Erdogan, rais wa Uturuki.
Recep Tayyip Erdogan, rais wa Uturuki. Reuters

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Alhamisi wiki hii amefungua mapambano mapya katika mgogoro wa kidiplomasia na Umoj wa Ulaya, akishtumu yombo vya seria vya Ulaya kuanzisha "kampeni" dhidi ya Uislamu baada ya kuachasheria inayoruhusu kampuni kupiga marufuku uvaaji wa hijabu kazini.

Matangazo ya kibiashara

"Je uko wapi uhuru wa dini? Nani alichukua uamuzi huo? Ni Mahakama ya Umoja wa Ulaya. Ndugu wapenzi, wameanzisha kampeni dhidi ya Uislamu, " Erdogan amesema Alhamisi wiki hii.

"Ulaya inarudi nyuma polepole kuelekeaa sikuza kabla ya Vita Vikuu vya II vya dunia," Bw Erdogan ameongeza.

Katika uamuzi wake Jumanne Machi 14, ECJ ilibaini kwamba kampuni inaweza kupiga marufuku katika sheria yake ya ndani alama yoyote inayoonekana ya kidini kama vile hijabu za Kiislamu.

Uturuki na Umoja wa Ulaya wanapitia mgogoro mbaya wa kidiplomasia katika miaka ya hivi karibuni, Ankara ikiwa na hasira kutokana na kukataliwa kwa baadhi ya nchi za Ulaya kuruhusu mikutano ya kampeni kuhusu kura ya maoni ya Aprili 16kwa minajili ya kuimarisha madaraka ya Rais Erdogan, ambaye ameyataja maamuzi haya kama maamuzi ya kiimla.