UFARANSA-SHAMBULIO-USALAMA

Ufyatuliaji risasi katika Shule ya Tocqueville Grasse nchini Ufaransa watu 8 wajeruhiwa

Mwanamke huyu akiondolewa na maafisa wa Idara za huduma za dharura baada ya kupigwa risasi katika shule ya sekondari ya Tocqueville Grasse, Alhamisi, Machi 16, 2017, ambapo watu 8 walijeruhiwa.
Mwanamke huyu akiondolewa na maafisa wa Idara za huduma za dharura baada ya kupigwa risasi katika shule ya sekondari ya Tocqueville Grasse, Alhamisi, Machi 16, 2017, ambapo watu 8 walijeruhiwa. REUTERS/Eric Gaillard

Ufyatuliaji risasi uliyoendeshwa na mwanafunzi mmoja katika shule lake la kusini-mashariki mwa Ufaransa, ambalo liliwajeruhi watu wanane unaonekana kuwa ni kitendo cha uwendawazimu cha kijana aliyetawalia na silaha," amesema Waziri wa Elimu Najat Vallaud-Belkacem.

Matangazo ya kibiashara

Serikali imetangaza hali ya tahadhari ya shambulizi baada risasi kusikika kusini mwa Ufaransa, Alhamisi hii Machi 16, 2017. Watu wanane, ikiwa ni pamoja na mwalimu mkuu wa shule hiyo wamejeruhiwa.

Nia ya mwanafunzi huyo "inaonekana kuhusiana mahusiano yake mabaya" na wanafunzi wengine, amesema mwendesha mashitaka.

Mwanafunzi wa miaka 17 aliyekua karibu na shule hilo ambaye alikamatwa, alikuwa amejihami kwa silaha za kivita. "Shule zote za mji wa Grasse (Alpes-Maritimes) zimefungwa kufuatia shambulio hilo," Msimamizi wa shule katika mkoa wa Nice ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mwanafunzi aliyekamatwa alikua amejihami kwa bunduki, bunduki ndogo mbilina guruneti mbili baada ya shambulio hilo la risasi katika shule ya sekondari mjini Grasse. Kwa taarifa za kwanza za uchunguzi, watu wanane wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na mwalimu mkuu. Awali mshirika katika shambulio hilo aliyetimka alitajwa. Mtuhumiwa aliyekamatwa alitekeleza kitendo hicho peke yake.

"Shule zote za mji huo zimefungwa baada ya shambulio hilo," ametangaza kwenyeTwitter Emmanuel Ethis, msimamizi wa shule katika mkoa wa Nice, ambaye pia amewataka wazazikuwa watulivu na kutokwenda karibu na shule wanakosomea watoto zao, huku akihakikisha kwamba "wanafunzi wako salama. "

Shambulio hilo lilitokea wakati wa mchana. Hali hiyo ilisababisha wanafunzi pamoja na walimu kuwa na wasiwasi mkubwa.

Serikali ya Ufaransa nayo ilituma onyo la shambulizi la kigaidi kupitia mtandao wake wa simu.

Mji wa Grasse ulio maarufu kwa kutengeneza marashi, uko umbali wa kilomita 44 kutoka mji wa Nice, ambapo lori lilitumiwa kufanya shambulizi mwezi Julai na watu 86 waliuawa.