Ufaransa

Safari za ndege zaanza tena Orly Paris baada ya shambulizi

Uwanja wa ndege wa Orly jijini Paris Ufaransa
Uwanja wa ndege wa Orly jijini Paris Ufaransa REUTERS/Charles Platiau

Safari za ndege katika uwanja wa ndege wa Orly jijini Paris nchini Ufaransa zimeanza kurejea kama kawaida leo Jumapili siku moja baada ya mtu aliyesababisha tahadhari kubwa ya usalama na vurugu za usafiri wakati alipomshambulia na askari kabla ya kupigwa risasi na kufa.

Matangazo ya kibiashara

Wapelelezi wa Kupambana na ugaidi leo Jumapili wamemwachia baba wa mshambuliaji huyo lakini wanaendelea kumshikilia kaka yake na binamu yake ili kupata taarifa za kumhusu Ziyed Ben Belgacem, mwenye umri wa miaka 39 raia wa Ufaransa.

Watu hao watatu wa familia walijipeleka wenyewe kwa polisi , mwendesha mashtaka wa Paris Francois Molins amewaambia waandishi wa vyombo vya habari mwishoni mwa siku ya Jumamosi.

Ziyed Ben Belgacem, ambaye alipigwa risasi na askari jana Jumamosi katika uwanja wa ndege wa Orly jijini Paris ameelezwa kuwa alikuwa tayari ā€œkufa kwa ajili ya Allahā€ na aliapa kuua wengine.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 39 mzaliwa wa Paris aliua wawakati alipo mshambulia askari, kumkabili na kujaribu kuiba silaha yake , na kukomesha saa kadhaa za vurugu.

Ā