MAREKANI-UINGEREZA-USALAMA

Marekani na Uingereza zapiga marufuku laptopu ndani ya ndege kutoka nchi 6

London inapiga marufuku abiria kusafiri ndani ya ndege na Laptops vifaa vingine vya elektroniki kutoka nchi tano za Kiarabu na Uturuki.
London inapiga marufuku abiria kusafiri ndani ya ndege na Laptops vifaa vingine vya elektroniki kutoka nchi tano za Kiarabu na Uturuki. AFP

Baada ya Marekani, Serikali ya Uingereza imetangaza marufuku kwa vifaa vingi vya eletroniki kwa abiria wanaosafiri kutoka mataifa sita yenye Waislamu wengi.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa nchini Uingereza wanasema kuwa marufuku hiyo inahusu abiria wanaosafiri kutoka Uturuki, Lebanon, Jordan, Misri, Tunisia na Saudia Arabia, wakielekea moja kwa moja nchini Uingereza.

Marufuku hiyo iliyochukuliwa na Uingereza pia inazuia vifaa kama tabiti na vifaa vya kucheza muziki vya kutumia DVD sawa na marufuku iliyotangazwa na Marekani.

Awali Maafisa wa Marekani walisema kuwa mabomu yanaweza kufichwa ndani vifaa kadhaa, hasa vifaa vya elektroniki.

Serikali ya Uingereza ilisema kuwa hii inafuatia mazungumzo yanayohusu usalama wa safari za ndege, ikisema kuwa marufuku hiyo inahitajika.