UINGEREZA

Taharuki nje ya bunge la Uingereza baada ya Afisa wa Polisi kuvamiwa

Afisa wa Polisi jijini London akiweka uzio katika eneo la tukio Machi 22 2017
Afisa wa Polisi jijini London akiweka uzio katika eneo la tukio Machi 22 2017 REUTERS/Stefan Wermuth

Afisa Polisi aliyekuwa amesimama mbele ya bunge la Uingereza amevamiwa na kudungwa kisu Jumatano jioni.

Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa Bunge nchini humo umethibitisha kutokea kwa tukio hili, na kuwataka wafanyakazi wa bunge kutoondoka nje ya jengo hilo hadi hali itakapokuwa salama zaidi.

Baadhi ya wabunge na walioshuhudia tukio hilo wamesema wamesikia milio minne ya risasi na kelele nje ya bunge hilo.

Tukio hili limesababisha kukwama kwa hali ya usafiri katika barabara zinazopakana na bunge huku maafisa wa usalama wakiendelea na msako zaidi.

Ripoti zinasema kuwa mtuhumiwa wa uvamizi huo amepigwa risasi.

Pamoja na hilo, ripoti kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu katika barabara ya Downing Street zinasema kuwa kiongozi huyo yuko salama