UFARANSA-FILLON-SIASA-HAKI

Fillon amtuhumu Hollande kuingilia kesi yake mahakamani

François Fillon katika makala ya kisiasa kwenye televisheni ya France 2, Alhamisi tarehe 23 Machi.
François Fillon katika makala ya kisiasa kwenye televisheni ya France 2, Alhamisi tarehe 23 Machi. THOMAS SAMSON / AFP

François Fillon ambaye alikua amealikwa kushiriki katika makala ya kisiasa kwenye televisheni ya France 2 Alhamisi wiki hii alimtuhumu rais wa Ufaransa François Hollande kupanga habari za uongo katika vyombo vya habari kuhusu kesi yake mahakamani. Rais Hollande amelaani madai hayo, akisema kuwa ni uzushi.

Matangazo ya kibiashara

François Fillon ambaye anakabiliwa na kesi mbalimbali kwa miezi miwili sasa, na hali hiyo kuweka hatarini kuwania kwake katika kinyang'anyiro cha urais mwaka huu, alitaka kuonyesha Alhamisi kuwa kesi yake imetengenezwa kisiasa kwa minajili ya kumuangusha katika kinyang'anyiro hicho. "Ni miezi miwili sasa tangu vyombo vya habari vikitoa habari zinazonipaka matope," alisema alisem Bw Fillon. "Hali hii inanifanya kufikiria Pierre Bérégovoy," ameongeza François Fillon, akimaanisha Waziri Mkuu François Mitterrand, aliyechunguzwa katika kesi ya mkopo na ambayo alikuja kumalizika mwaka 1993. "Nimelewa kwa nini ninaweza kukabiliwa na hali hii, "Bw Fillon alisema.

Siku moja baada ya ushahidi wa kwanza, François Fillon alishtumiwa kosa la "kushambulia vyombo vya habari" na kisha "mapinduzi ya kitaasisi." Lakini siku ya Alhamisi, katika makala ya kisiasa kwenye televisheni ya France 2, mgombea wa mrengo wa kulia na kati katika uchaguzi wa urais aliendelea kukanusha tuhuma dhidi yake, akinyooshea kidole cha lawamaviongozi wa ngazi ya serikalini.

Kwa mujibu wa François Fillon, mwanzilishi wa madai haya ambayo yanaendelea kuongezeka kila kukicha tangu mwishoni mwa mwezi Januari si mwingine ispokua François Hollande.

Hata hivyo Rais wa Ufaransa François Hollande amekanusha madai hayo na kusem akuwa ni uzushi mtupu.