UINGEREZA-USALAMA

London yamtambua mshambuliaji wa Westminster

Mishumaa iliwashwa moto na shada za maua ziliwekwa katika eneo la tukio la Trafalgar Square, Alhamisi, tarehe 23 Machi, kwa kutoa heshimakwa wahanga wa shambulizi lililiendeshwa karibu na Bunge la Uingereza.
Mishumaa iliwashwa moto na shada za maua ziliwekwa katika eneo la tukio la Trafalgar Square, Alhamisi, tarehe 23 Machi, kwa kutoa heshimakwa wahanga wa shambulizi lililiendeshwa karibu na Bunge la Uingereza. REUTERS/Hannah McKay

Polisi wa Uingereza imemtambua mshambuliaji ambaye alisababisha vifo vya watu wanne na kuwajeruhi wengine arobaini mjini London siku ya Jumatano. Shambulizi ambalo lilidaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State (IS).

Matangazo ya kibiashara

Polisi ya Ungereza imebaini kwamba mtu ni raia wa Uingereza ambaye anajulikana kwa jina la Khalid Masood, mwenye umri wa miaka 52.

Masood, alizaliwa Desemba 25, 1964 katika jimbo la Kent (kusini mwa Uingereza), aliishi hivi karibuni katika jimbo la West Midlands (katikati mwa Uingereza) na "hakua kwenye orodha ya watu wanaofanyiwa uchunguzi unaoendelea," Idara ya ujasusi ya Uingereza (Scotland Yard) ilisema siku ya Alhamisi . "Idara ya Ujasusi haikuwa na ushahidi wowote kwamba Khalid Masood aneliweza kuendesha shambulizi hilo la kigaidi."

Mamia ya watu walikusanyika Alhamisi usiku katika eneo la Trafalgar Square, eneo muhimu lililo katikati ya mji mkuu wa Uingereza, kwa ajili ya kukesha kwa kuwakumbuka wahanga wa shambulio hilo lililotokea siku ya Jumatano. "Wakazi wa London hawatokubali kutishwa na ugaidi," Meya wa mji wa London Sadiq Khan aliahidi.

Ujumbe, bendera na shada za maua vilipelekwa na umati wa watu katika eneo la shambulizi ambalo limewkwa chini ya ulinzi mkali wa polisi. Watu walitoa rambirambi zao kwa maafisa wa polisi waliopoteza mwenzao katika shambulio hilo.

Jumatano Khalid Masood alitumia gari lake kwa kugonga umati wa watu kwenye daraja la Westminster, karibu na eneo la Big Ben, na kuua watu wawili, Mmarekani wa miaka hamsini na raia mmoja wa Uingereza mwenye asili ya Uhispania na kuwajeruhi watu wengi.