EU

Umoja wa Ulaya waadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake

Bendera ya Umoja wa Ulaya
Bendera ya Umoja wa Ulaya REUTERS/Yves Herman

Umoja wa Ulaya unaadhimisha miaka 60 tangu kuundwa kwake huku viongozi wa Mataifa hayo wakitarajiwa kurejelea tena viapo vya kuendelea kushirikiana na kuimarisha muungano huo.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wa Mataifa 27 ya Umoja huo ukiondoa Uingereza, wanakutana mjini Rome nchini Italia siku ya Jumamosi kuthathmini hatua zilizopigwa katika Umoja huo na changamoto zinazowakabili.

Miaka 60 iliyopita, wawakilishi wa Mataifa sita ambayo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani Magharibi, Italia, Luxembourg na Uholanzi walikutana mjini Rome na kutia saini mkataba wa kuanzisha Umoja huo ambao ulivutia mataifa mengine 28.

Ni maadhimisho yanayofanyika karibu mwaka mmoja baada ya Uingereza kujiondoa katika Umoja huo.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis akizungumza na viongozi wa Umoja huo siku ya Ijumaa, aliwataka kuja na malengo mapya na kuimarisha umoja wao kuepuka mgawanyiko katika siku zijazo.

Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis Machi 25 2017 mjini Rome, Italia
Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya na Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis Machi 25 2017 mjini Rome, Italia REUTERS/Andrew Medichini

Marekani nayo imepongeza hatua ya Umoja wa Ulaya kuadhimisha miaka 60 tangu kuundwa kwake.

Pongezi za Trump zinakuja baada ya kuonekana kutounga mkono Umoja huo na kupongeza hatua ya Uingereza kujiondoa.

Mafanikio ya EU
Mataifa ya Umoja huo yana watu Milioni 510.

Umoja huu umefanikiwa kuwa na sarafu moja inayofahamika kama Euro ambayo imekuwa ikitumika tangu mwaka 2002.

Imefanikiwa katika uhuru wa watu kufanya kazi na kutembea katika mataifa yote 27 bila ya vikwazo vyovyote.

Ushirikiano wa maswala ya usalama.

Soko huria la kuuza na kununua bidhaa mbalimbali.

Fahamu nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya:- Austria, Ubelgiji, Bulgaria, Croatia, Cyprus, Jamhuri ya Czech , Denmark, Estonia, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ugiriki, Hungary, Ireland, Italia,Latvia, Lithuania, Luxembourg, Malta, Uholanzi, Poland, Ureno, Romania, Slovakia, Slovenia, Uhispania na Sweden