RFI-FRANCE 24

RFI na France 24 zaomboleza kifo cha mwanahabari wake maarufu Laurent Sadoux

Radio France International (RFI)  na France 24 inaomboleza kifo cha Mtangazaji wake maarufu Laurent Sadoux aliyefariki dunia siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 51.

Laurent Sadoux, wakati wa uhai wake akiwa RFI
Laurent Sadoux, wakati wa uhai wake akiwa RFI ®Pierre René-Worms/RFI
Matangazo ya kibiashara

Sadoux aliugua muda mfupi kabla ya kufariki kwake, kifo ambacho kimeleta huzuni kubwa kwa wafanyikazi wenzake na kila mmoja aliyemfahamu.

Alikuwa mtangazaji wa vipindi vya historia lakini pia mtangazaji wa Habari za bara Afrika kwa lugha ya Kifaransa.

Atakumbukwa kuwa mwanahabari mwenye weledi mkubwa aliyefahamu vema historia na kufuatilia kwa karibu matukio mbalimbali kutoka barani Afrika.

Wakati wa uhai wake, aliwahi kuishi jijini Bujumbura nchini Burundi na kutangamana na raia wa nchi hiyo na hata kujitengezea marafiki.

Mkurugenzi Mkuu wa RFI na France 24 Cecile Megie amesema kifo cha Sadoux ni pigo kubwa na kuongeza kuwa atakumbukwa daima.

Wasikilizaji wa RFI na watazamaji wa France wataikosa sauti yake ya kuvutia na mtindo wake wa kusoma taarifa za Habari.