Pata taarifa kuu
SWEDEN

Maafa nchini Sweden baada ya Lori kugonga mkusanyiko wa watu jijini Stockholm

Hali ilivyokuwa baada ya Lori kuwagonga watu nchini Sweden
Hali ilivyokuwa baada ya Lori kuwagonga watu nchini Sweden Reuters
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
1 Dakika

Lori limegonga mkusanyiko wa watu katikati ya jiji la Stockholm nchini Sweden na kusababisha maafa na majeruhi.

Matangazo ya kibiashara

Nina Odermalm Schei, msemaji wa wa idara ya Inteljensia nchini humo ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa watu wamepoteza maisha lakini hakutoa idadi.

Waziri Mkuu Stefan Lofven amesema tukio hilo ni la kigaidi na kusababisha vifo vya watu watatu.

Ripoti zinasema kuwa Lori hilo lilikuwa limeibwa baada ya kuwasilishwa kwa wamiliki wa hoteli moja.

Walioshuhudia tukio hilo la Ijumaa jioni wanasema lilikuwa na kuogofya sana.

Uongozi wa mji huo umetangaza kusitishwa kwa safari za treni katika mji huo.

Hakuna kundi ambalo limejitokeza kudai kuhusika na shambulizi hilo.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.