UJERUMANI-USALAMA

Polisi nchini Ujerumani wachunguza kushambuliwa kwa basi la Borrusia Dortmund

Basi la Borussia Dortmund baada ya kushambuliwa
Basi la Borussia Dortmund baada ya kushambuliwa Reuters / Kai Pfaffenbach

Polisi nchini Ujerumani wanaendelea na msako wa kuwatafuta washukiwa waliohusika na milipuko mitatu iliyolenga basi lililokuwa limewabeba wachezaji wa klabu ya soka ya Borussia Dortmund na kusababisha mchezaji mmoja kujeruhiwa, Jumanne usiku.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti za awali zinasema kuwa halikuwa shambulizi la kigaidi lakini lililenga timu hiyo.

Barua ilipatikana karibu na eneo ambalo shambulizi hilo lilitokea, lakini polisi wanasema haina maelezo ya kutosha.

Katika tukio hilo Mchezaji mmoja wa Dortmund na raia wa Uhispania Marc Bartra amejeruhiwa na kufanyiwa upasuaji.

Inadaiwa kuwa huenda mashabiki ambao ni wapinzani wa Borrusia Dortmund ndio waliohusika.

Baada ya kutokea kwa shambulizi hilo, mchuano wa klabu bingwa kati ya Borrusia Dortmund na Monaco ya Ufaransa umeahirishwa na sasa utachezwa leo Jumatano.