UJERUMANI-BORRUSIA DORTMUND

Mshukiwa aliyekamatwa hakuhusika na shambulizi la Borrusia Dortmund

Polisi nchini Ujerumani
Polisi nchini Ujerumani Wikipedia

Viongozi wa Mashtaka nchini Ujerumani wanasema hawana ushahidi unaomhusisha mshukiwa wa shambulizi la basi la wachezaji wa klabu ya Borrusia Dortmund kuwa, yeye ndiye aliyehusika.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, wameomba Mahakama kuendelea kumshikilia raia huyo wa Iraq mwenye umri wa miaka 26 ili kumhoji zaidi.

Abdul Beset A, anaendelea kushukiwa kuwa mfuasi au kushirikiana na kundi la kigaidi la Islamic State.

Ripoti zinasema kuwa alikuwa mmoja wa Makamanda wa kundi hilo nchini Iraq mwaka 2014 na alihusika katika utekaji  nyara na mauaji.

Anatarajiwa kufikishwa Mahakamani baadaye siku ya Alhamisi na kufunguliwa mashitaka ya kuhusika na shambulizi la basi hil.

Raia mwingine wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 28, anahusishwa lakini hajakamatwa.