UFARANSA-SIASA

Raia wa Ufaransa wanapiga kura kumchagua rais

Mgombea wa urais Emmanuel Macron alipiga kura mapema Aprili 23 2017
Mgombea wa urais Emmanuel Macron alipiga kura mapema Aprili 23 2017 Eric FEFERBERG / POOL / AFP

Raia wa Ufaransa wanapiga kura kumchagua raia mpya.

Matangazo ya kibiashara

Usalama umeimarishwa kote nchini humo kuhakikisha kuwa zoezi hili linafanyika na kumalizika salama.

Wapiga kura Milioni 47 wanaamua ni nani atakayemrithi rais Francois Hollande ambaye mwaka uliopita, alitangaza kutotetea nafasi yake.

Wagombea 11 wanatafuta wadhifa huo. Wachambuzi wanasema kuwa kutakuwa na mchuano mkali na kuna uwezekano mkubwa wa kutopatikana kwa mshindi katika mzunguko wa kwanza.

Aidha, wadadidi hao wanaeleza kuwa ushindani mkali zaidi utakuwa kati ya mgombea binafsi Emmanuel Macron, na mgombea wa chama cha Front National Bi. Marine Le Pen.

Ni Uchaguzi unaoangaziwa kwa karibu sana kote duniani, hasa baada ya baada ya mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini Marekani baada ya Donald Trump kuibuka mshindi lakini pia Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Watano hao ni pamoja na François Fillon kutoka chama cha Les Republicains, Benoît Hamon kutoka chama cha Kisosholisti, Marine Le Pen kutoka mrengo wa Front National, Emmanuel Macron ambaye ni mgombea binafsi na Jean-Luc Mélenchon kutoka chama cha La France insoumise.

Hata hivyo, wachambuzi nchini humo wanasema kuwa Marine Le Pen na Emmanuel Macron huenda wakamaliza katika nafasi ya kwanza na ya pili na kumenyana katika mzunguko wa pili.