Habari RFI-Ki

Macron na Lepen kuumana katika duru ya pili ya Uchaguzi Ufaransa

Sauti 09:35
Emmanuel Macron na Marie Le Pen watachuana katika duru ya pili ya uchaguzi nchini Ufaransa
Emmanuel Macron na Marie Le Pen watachuana katika duru ya pili ya uchaguzi nchini Ufaransa

Karibu katika makala ya habari rafiki leo tunaangazia uchaguzi mkuu nchini Ufaransa,kwa mara ya kwanza katika historia ya jamuhuri ya Ufaransa mgombea wa kiti cha uraisi asiyewakilisha chama cha siasa anapata uungwaji mkono chini ya vuguvugu la mabadiliko.Emmanuel Macron mgombea wa mrengo wa kati na Marine Le Pen wa chama cha kihafidhina wanaongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais uliofanyika jana nchini Ufaransa na sasa watachuana vikali katika duru ya pili ya uchaguzi huo unaopangwa kufanyika Mei 7 mwaka huu.