MAKEDONIA-USALAMA

Waandamanaji washambulia majengo ya Bunge Makedonia

Zoran Zaev, kiongozi wa upinzani kutoka mrengo wa kushoto nchini Makedonia, katika hotuba yake wakati wa maandamano dhidi ya serikali. Skopje, Mei 17, 2015.
Zoran Zaev, kiongozi wa upinzani kutoka mrengo wa kushoto nchini Makedonia, katika hotuba yake wakati wa maandamano dhidi ya serikali. Skopje, Mei 17, 2015. REUTERS/Ognen Teofilovski

Waandamanaji wamevamia majengo ya bunge nchini Makedonia baada ya kuchaguliwa kwa Spika kutoka kwenye kabila la Albania. Hali ya machafuko imeendelea kushuhudiwa nchini humo kufuatia maandamano yanayoendelea.

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano yalizuka na kusababisha majeruhi ya watu 10 wengi wakionekana kutokwa na damu.

Kiongozi wa chama kilicho na wabunge wengi Zoran Zaev, pia alijikuta katika vurugu hizo na kujeruhiwa vibaya.

Kumekuwa na maandamano ya wiki kadhaa kushinikiza kuitishwa kwa uchaguzi mpya.