Wasifu wa Macron

Mfahamu Emmanuel Macron

Rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron
Rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron REUTERS/Benoit Tessier

Emmanuel Macron ni rais wa kwanza kijana duniani, alizaliwa Desemba 21, 1977 katika mji wa Amiens, ulioko kaskazini mwa Ufaransa, ambapo miaka ya 1990 alijiunga na taasisi mbali mbali za benki nchini Ufaransa. Macron alifunga na Mke wake bi Brigitte Trogneux Macron, mwenye umri wa miaka 64 Oktoba 20, mwaka 2007.

Matangazo ya kibiashara

Macron Alisoma katika Shule inayotoa mafunzo ya Utawala (ENA) ambapo alipata Diploma mwaka wa 2004, akawa mkaguzi wa mahesabu ya fedha za serikali, kabla ya kuanzisha shughuli za biashara akishirikiana na taasisi kubwa ya kubadilisha pesa ifahamikayo kama Rothschild & Cie mwaka 2008.

Macron Alijiunga na chama cha kisoshalisti PS mwaka 2006-Hadi 2009, ambapo kama mwanachama aliteuliwa kama naibu katibu mkuu katika ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Ufaransa chini ya utawala wa rais François Hollande mwaka 2012.

Baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Uchumi na Viwanda, ambapo kama mtu mwenye uzoefu katika masuala ya fedha kwenye Wizara hii aliyoisimamia alipewa jukumu la kushughulikia mahesabu ya fedha za Serikali baada ya waziri mkuu wa wakati huo Manuel Valls kufanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri kwa mara ya pili mnamo mwaka 2014.

Emmanuel Macron alikua waziri wa uchumi mwenye umri mdogo tangu mwanasiasa Valery Giscard d'Estaing ashike wadhifa huo.

Kama waziri wa uchumi Emmanuel Macron alikuwa mshauri wa karibu wa rais Francois Hollande wa masuala ya uchumi, akawa mmoja wa wanasiasa wa chama cha kisoshalisti walioanzisha mikataba ya mikopo ya kodi mwaka huo wa 2014.

Mwezi Aprili mwaka 2016, Emmanuel Macron alianzisha harakati zake za kisiasa, baada ya kutangaza kujiuzulu kwake kwenye wadhifa huo miezi minne baadaye, ambapo aliamua kukihama chama hicho cha kisoshalisti, na kuanzisha vuguvugu huru la kisiasa.

Katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa Ufaransa 2017, Macron alifanikiwa kupata asilimia 24, 01 ya kura zote akiwa mbele ya mpinzani wake mwenye msimamo mkali na mgombea kwa tiketi ya chama cha FN Marine Le Pen.

Na hivyo wagombea hao wawili walifanikiwa kupenya na kuingia katika duru la pili la uchaguzi wa Mei 7 mwaka huu na hatimaye Emmanuel Macron ameibuka kuwa mshindi kwa kujizolea asilimia 65.1 ya kura zote.