UFARANSA-UCHAGUZI

Sarafu ya Euro yaimarika baada ya ushindi wa Emmanuel Macron

Jedwali linaloonesha namna sarafu ya Euro ilivyoimarika dhidi ya sarafu ya Dola ya Marekani Mei 7 2017
Jedwali linaloonesha namna sarafu ya Euro ilivyoimarika dhidi ya sarafu ya Dola ya Marekani Mei 7 2017 theguardian.com

Thamani ya sarafu ya Euro imeimarika dhidi ya sarafu ya Dola ya Marekani kwa mara ya kwanza kwa muda wa miezi sita, kutokana na ushindi wa Emmanuel Macron kuwa rais mpya wa Ufaransa. 

Matangazo ya kibiashara

Masoko mengi ya fedha yamebadilisha Euro moja kwa Dola 1.102 kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi wa Marekani mwezi Novemba mwaka uliopita.

Waekezaji na wanauchumi wamefurahishwa na ushindi wa Macron ambaye anaunga mkono Umoja wa Ulaya na utumishi wa sarafu ya Euro.

Aidha, sarafu ya Euro imeimarika dhidi ya sarafu kutoka Japan ya Yen kwa asilimia 0.3 hali iliyoonekana pia kwa Pound ya Uingereza.

Wachambuzi wa maswala ya Uchumi wanasema ushindi wa Macron unaonesha kuwa wanasiasa wanaounga mkono Umoja wa Ulaya na matumizi ya sarafu ya Euro, wana nafasi kubwa ya kushinda Uchaguzi katika mataifa mbalimbali ya Ulaya.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Ulaya Jean Claude Juncker amesema ushindi wa Macron, ni ushindi wa Umoja wa Ulaya.