UCHAGUZI UFARANSA 2017

Ufaransa: Asilimia 65.30 wajitokeza kupiga mpaka kufikia jioni hii tofauti na 2012

Idadi ya raia waliojitokeza kupiga kura mpaka kufikia mchana kwa saa za Paris ilikuwa asilimia 28.23 ikiwa ni chini ya kiwango kabisa ukilinganisha na hatua kama hii mwaka 2012.

Wananchi wa Ufaransa wakiwa kwenye mstari kupiga kura kwenye uchaguzi wa duru ya pili
Wananchi wa Ufaransa wakiwa kwenye mstari kupiga kura kwenye uchaguzi wa duru ya pili REUTERS/Emmanuel Foudrot
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo mpaka kufikia saa kumi na mbili kamili kwa saa za Afrika Mashariki idadi ilikuwa ni asilimia 65.30.

Kwenye eneo moja ambalo mgombea Emmanuel Macron alipiga kura kiwango kilikuwa chini kutokana na sababu za kiusalama.

Mpaka kufikia mchana idadi ilikuwa ni asilimi 30.66 kwenye uchaguzi wa mwaka 2012 kwenye duru ya pili ikiwa nik chini kidogo hadi asilimia 28.54 kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

Idadi ya watu kushiriki kwenye uchaguzi mara nyingi nchinik Ufaransa huwa juu hasa kwenye uchaguzi wa urais ambao mara nyingi wapiga kura hujitokeza kwa zaidi ya asilimia 80.

Macron na mpinzani wake Marine Le Pen walipiga kura majira ya asubuhi kama alivyofanya rais anayemaliza muda wake Francois Hollande.

Katika hatua nyingine uwanja wa jumba la makumbusho la Louvre ulifungwa kwa muda kuruhusu jukwaa maalumu kuwekwa eneo ambalo mgombea Macron anatarajiwa kuzungumza baada ya matokeo rasmi kutangazwa.

Zaidi ya wanahabari 300 walilazimika kuondolewa kwenye eneo ambako jukwaa hilo lilikuwa linawekwa.

Uchaguzi huu umenyika huku nchik hiyo ikiwa chini ya hali ya hatari ambayo ilitangazwa mwezi Novemba mwaka 2015 baada ya shambulio la kigaidi la jijini Paris.

Polisi na wanajeshi zaidi ya elfu 50 wamesambazwa nchi nzima kutazama usalama wakati wa zoezi la kupiga kura.

Kwa mujibu wa taasisi mbalimbali za utafiti nchini Ufaransa zinaonesha kuwa idadi ya watu ambao hawakupiga kura pia imekuwa kubwa ambapo asilimia 26 ya wapiga kura inaelezwa kuwa hawakupiga kura kwenye uchaguzi huu ukilinganisha na ile iliyokuwa mwaka 2012.