UFARANSA-UCHAGUZI

Wafaransa wapiga kura kuchagua raisi leo

Montreal, Quebec, Wafaransa walipiga kura, Jumamosi, Mei 6, 2017.
Montreal, Quebec, Wafaransa walipiga kura, Jumamosi, Mei 6, 2017. REUTERS/Chris Wattie

Wapiga kura nchini Ufaransa wanachagua raisi atakayeongoza taifa hilo baada ya kampeni zilizoligawa taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Raia wa Ufaransa katika maeneo mbalimbali nje ya taifa hilo nao wameanza kupiga kura.

Wagombea waliofanikiwa kutinga duru ya pili ya uchaguzi Emmanuel Macron,mwenye umri wa miaka 39 anakabiliana na bi Marine Le Pen,mwenye umri wa miaka 48.

Vituo vilifunguliwa saa kumi na mbili kamili za asubuhi kwa saa za Ufaransa na vinatarajiwa kufungwa saa moja kamili usiku.

Aidha katika baadhi ya miji mikubwa vituo havitafungwa hadi saa mbili usiku ambapo matokeo ya awali ya uchaguzi yatatarajiwa kuanza kutolewa mara baada ya vituo kufungwa.

Zaidi ya wanausalama elfu hamsini wametawanywa nchini Ufaransa kuimarisha usalama wakati huu raia wakipiga kura kumchagua raisi mpya.

Hali ya tahadhari imeendelea kuchukuliwa nchini Ufaransa kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya November 2015,ambapo vikosi vya ulinzi na usalama nchini humo vinashirikiana na maafisa wa kupambana na ugaidi kuhakikisha hali inakuwa shwari katika takribani vituo elfu 66,546 vya kupigia kura.