UFARANSA-MACRON-ULINZI

Rais Macron na sera mpya katika ulinzi

Emmanuel Macron pamoja na François Hollande wakati wa maadhimisho ya Mei 8 mjini Paris.
Emmanuel Macron pamoja na François Hollande wakati wa maadhimisho ya Mei 8 mjini Paris. REUTERS/Francois Mori

Mkuu mpya wa majeshi ya Ufaransa atakabiliwa na changamoto kadhaa katika masuala ya ulinzi ikiwa ni pamoja na tatizo la ugaidi. Mapambano dhidi ya kundi la Islamic State ni moja ya mambo muhimu katika sera mpya ya ulinzi ya rais mteule Emmanuel macron.

Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi Rais mteule wa Ufaransa, Emmanuel macron aliapa kuendelea na mapambano dhidi ya kundi la Islamic.

Mapambano dhidi ya ugaidi bado ni kipaumbele

"Katika mapambano dhidi ya ugaidi, Ufaransa itakuwa katika mstari wa mbele katika ardhi ya Ufaransa na nje ya nchi," alisema Emmanuel Macron. Operesheni za sasa, Chammal Mashariki ya Kati, Barkhane katika ukanda wa Sahel zitabaki. Pamoja na askari wengi kwa jumla watasalia katika maeneo hayo.

Rais mpya alitembelea nchini Jordan kwa siri wakati alikuwa mgombea, na kwa haraka anatazamiwa na askari wa Kikosi cha Ufaransa cha Barkhane barani Afrika. Mkuu mpya wa majeshi pia ataelewana haraka na utawala wa Donald Trump kuhusu hali inayojiri katika mji wa Raqqa nchini Syria, mji ambapo wamejificha Wafaransa wengi wakijihadi.

Operesheni Sentinel kuzingatiwa

Kama alivyotaka rais Hollande baada ya mashambulizi ya mwaka 2015, operesheni ijulikanayo kwa jina la Sentinel yenye kikosi cha askari 7,000 nchini Ufaransa (hadi 10,000 wakati wa dharura) itaendelea kutekelezwa nchini kote Ufaransa. Tangu mwaka 2015, mara nane askari wa operesheni Sentinel walilengwa, hasa wakati wa mashambulizi kwa kisu.