UFARANSA-EU-UCHAGUZI

Nchi za Ulaya zampongeza na kumuunga mkono Emanuel Macron

Emmanuel Macron alipowasili katika makao makuu ya kampeni yake Mei 9, 2017.
Emmanuel Macron alipowasili katika makao makuu ya kampeni yake Mei 9, 2017. REUTERS/Gonzalo Fuentes

Rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macron ameendelea kupata uungwaji mkono kutoka kwa nchi za Ulaya ambazo ni washirika wa karibu wa Ufaransa siku moja tu baada ya kiongozi huyo kupata ushindi wa kishindo dhidi ya Marine Le Pen kwenye uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Tayari ikulu ya Marekani imethibitisha kuwa Macron atakutana na rais Donald Trump May 25 mwaka huu wakati wa mkutano wa nchi za muungano wa kujihami wa nchi za Magharibi, NATO.

Katika hatua nyingine katibu mkuu wa vuguvugu la En Marche lililofanikisha ushindi wa Macron, Richard Feron amesema wanabadili jina lao kutoka En Marche na sasa litafahamika kama Republique En Marche.

Baada ya ushindi wake wananchi wengi na wanasiasa wanasubiri kuona namna ambavyo kiongozi huyo atafanikiwa kuunda serikali au ikiwa atapata idadi ya wabunge anaopaswa kuwa nao ili vuguvugu lake liunde serikali.

Emmanuel Macron anatazamiwa kukabidhiwa madaraka Jumapili ijayo.