UFARANSA-SIASA

Mpwa wa Marine Le Pen aachana na siasa nchini Ufaransa

Marion Marechal-Le Pen mpwa wa aliyekuwa mgombea wa urais nchini Ufaransa Marine Le Pen.
Marion Marechal-Le Pen mpwa wa aliyekuwa mgombea wa urais nchini Ufaransa Marine Le Pen. Wikipedia

Marion Marechal-Le Pen mpwa wa aliyekuwa mgombea wa urais nchini Ufaransa Marine Le Pen, ametangaza kuachana na siasa baada ya Le Pen kushindwa. 

Matangazo ya kibiashara

Marion mwenye umri wa miaka 27 anakumbukwa kuwa mbunge mwenye umri mdogo baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 22, mwaka 2012.

Wachambuzi wa siasa nchini Ufaransa wanasema hatua hii kuelekea uchaguzi wa wabunge mwezi ujao , unaonesha kuwa kuna mgawanyiko katika uongozi wa chama hicho cha Front Nationale.

Wakati uo huo, sikumoja baada ya kutangaza dhamira yake ya kugombea ubunge kupitia vuguvugu la rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macron, aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Manuel Valls amesema chama chake cha Socialist kimekufa kisiasa.

Hata hivyo kauli ya Valls imepingwa vikali na waziri mkuu Bernard Cazeneuve ambaye amesema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha wanakirejesha chama hicho kwa nguvu kwenye siasa za nchi na ikiwezekana kuchukua viti zaidi kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Rais mteule Macron bado hajamtangaza waziri wake mkuu akisubiri kufanya hivyo siku ya Jumapili baada ya kukabidhiwa madaraka kutoka kwa rais Francois Hollande.