UFARANSA-UCHAGUZI

Zaidi ya wagombea 428 kuwania uchaguzi wa wabunge kwa tiketi ya chama cha Macron

Katibu Mkuu wa chama cha Republique en Marche, Richard Ferrand, akiikutana na waandishi wa habari Mei 11, 2017 aipokua akiwasilisha orodha ya wagombea katika tiketi ya chama cha Emmanuel Macron katika uchaguzi wa wabunge.
Katibu Mkuu wa chama cha Republique en Marche, Richard Ferrand, akiikutana na waandishi wa habari Mei 11, 2017 aipokua akiwasilisha orodha ya wagombea katika tiketi ya chama cha Emmanuel Macron katika uchaguzi wa wabunge. Eric FEFERBERG / POOL / AFP

Siku ya Alhamisi Mei 11, chama cha Emmanuel Macron cha Republique en Marche kimetoa orodha ya kwanza ya wagombea 428 katika uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanyika tarehe 11 na 18 June. Manuel Valls, aliyekua waziri mkuu katika utawala wa Rais Francois Hollande hayumo katika orodha hiyo

Matangazo ya kibiashara

Chama cha Republique en Marche (LREM) kimetoa orodha hiyo ambapo nusu ya wagombea ni wanawake, na 52% ni kutoka vyama vya kiraia.

Katibu Mkuu wa chama cha Republique en Marche, Richard Ferrand, pia amesema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba chama chao hakitakua na mgombea dhidi ya Manuel Valls katika jimbo lake, hata kama waziri mkuu huyo wa zamani hakamilishi vigezo kwa kuteuliwa na chama cha Emmanuel Macron. Alihudumu mihula mitatu mfululizo ya ubunge wakati ambapo ni kinyume na sheria za uteuzi katika chama cha Republique en Marche. Lakini Emmanuel Macron hana haja ya kumdharau waziri mkuu wa zamani na ameamua kutoteua mgombea dhidi yake.

Wagombea wa mwisho 149 kuteuliwa ifikapo Mei 17

Richard Ferrand ameongeza kuwa 93% ya wagombea wanafanya kazi mpaka sasa. Umri wa wastani wa wagombea ni miaka 46, alisema. "Tuna lengo la kujenga idadi kubwa ya mabadiliko na hivyo kupata kundi la wabunge kwa chama cha Republique en Marche, idadi kubwa ya wabunge katika Bunge la taifa," alisema Richard Ferrand.