UFARANSA-UCHAGUZI

Emmanuel Macron kuapishwa hii leo

Emmanuel Macron,rais mteule wa Ufaransa
Emmanuel Macron,rais mteule wa Ufaransa REUTERS/Philippe Wojazer

Rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macron ataapishwa leo Jumapili kuongoza nchi hiyo, akiwa rais wa kwanza mwenye umri mdogo kuwahi kuongoza taifa hilo

Matangazo ya kibiashara

Kuapishwa kwa Macron kunakuja huku akiwa anakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kufufua uchumi na kuleta pumzi mpya ya uhai ndani ya umoja wa Ulaya

Macron anaapishwa kuchukua nafasi ya rais anayemaliza muhula wake Fancois Hollande ambaye miaka yake mitano madarakani ilikumbwa na ukosefu mkubwa wa ajira na mashambulizi ya kigaidi.

Baada ya kupita katika zulia jekundu katika Ikulu ya Elyzee katikati mwa jiji la Paris, Macon na Hollande watakuwa na mazungumzo ya faragha katika ofisi ya rais ambako Macron atakabidhiwa namba za kufungua silaha za Nuclear za Ufaransa