UFARANSA-UJERUMANI-USHIRIKIANO

Merkel na Macron: Tuko tayari kubadili mkataba kwa mageuzi ya Ulaya

Angela Merkel na Emmanuel Macron wanasema wako tayari kwa marekebisho ya mkataba kwa mageuzi ya Ulaya.
Angela Merkel na Emmanuel Macron wanasema wako tayari kwa marekebisho ya mkataba kwa mageuzi ya Ulaya. AFP

Siku moja baada ya kukabidhiwa madaraka na kutawazwa kama rais wa Ufaransa, Emmanuel macron amezuru Ujerumani siku ya Jumatatu Mei 15 na kupokelewa na mwenyeji wake Angela Merkel.

Matangazo ya kibiashara

Lengo la ziara hiyo ni kuendeleza na kuimarisha uhusiano kati ya Ufaransa na Ujerumani, nchi mbili wanachama wa Umoja wa Ulaya, ambao unaonekana kukabiliwa na hali ya sintofahamu.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais huyo mpya wa Ufaransa walisema kuwa  ikiwa ni lazima kwa wazo la mabadiliko ya mikataba kwa ajili ya mageuzi ya Ulaya inayokabiliwa na mgogoro wa kupanda kwa chuki na ukabila.

"Kwa mtazamo wa Ujerumani, inawezekana kubadili mikataba kama itakua ni muhimu," alisema Angela Merkel kwa vyombo vya habari mjini Berlin, wakati ambaporais mteule wa UfaransaEmmanuel Macron alisema kwa upande wake, "hakuna mwiko" dhidi ya wazo hili.

"Suala la mabadiliko ya mkataba lilikuwa mwiko kwa Ufaransa, katika utawala wangu halitakua mwiko," rais Macron alisema.

Viongozi hawa wawili walijieleza baada ya mkutano wao wa kwanza katika mji mkuu wa Ujerumani tangu kuchaguliwa kwa Emmanuel Macron kama rais wa Ufaransa.

Emmanuel Macron aliwasili mjini Berlin siku ya Jumatatu, Mei 15, ambapo, pamoja na baadhi ya tofauti kuhusu masuala kama vile mageuzi ya mikataba ya Umoja wa Ulaya, alithibitisha nafasi ya uongozi wa Ufaransa na Ujerumani katika Umoja huo ambao unakabiliwa na mgogoro unaohitaji kutafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Siku moja baada ya kutawazwa na mara tu baada ya kumteua waziri wake mkuu, Edouard Philippe, rais mteule wa faransa alizuru mji mkuu wa Ujerumani, Berlin ambao alichagua kwa safari yake ya kwanza ya kirais nje ya nchi, kama walivyofanya watangulizi wake Nicolas Sarkozy au François Hollande kabla yake.

Baada ya kupokelewa na mwenyeji wake Angela Merkel, Emmanuel Macron na Angela Merkel walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kabla ya kuchangia chakula cha jioni.

"Atatetea maslahi ya Ufaransa, nitatetea maslahi ya Ujerumani lakini nina uhakika kutakuwa na pointi nyingi ambazo tutaafikiana " ikiwa ni pamoja na ushirikiano ambao utawezekana, Bi Merkel alisema saa chache kabla ya mkutano huo.