MACEDONIA-SIASA

Rais wa Macedonia akubali upinzani kuunda serikali

Rais wa Macedonia Gjorge Ivanov akizungumza na wanahabari
Rais wa Macedonia Gjorge Ivanov akizungumza na wanahabari REUTERS/Ognen Teofilovski

Rais wa Macedonia amekubali  chama cha upinzani nchini humo, SDSM kuunda serikali miezi mitano baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu .

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya rais Gjorge Ivanov imekuja baada ya chama hicho kinachoongozwa na Zoran Zaev, kushinda Uchaguzi wa wabunge.

Awali, rais huyo alikuwa amekataa kutoa ruhusu kwa upinzani kuunda serikali na kukabidhi madarakani kwa amani kwa hofu kuwa huenda serikali yao ingezua vita na kuharibu umoja wa nchi hiyo.

 

Taifa hilo linalotaka kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya na umoja wa jeshi la NATO, limekuwa katika mvutano mkubwa wa kisiasa kwa muda wa miaka miwili kutokana na kashfa mbalimbali.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema hatua ya Spika wa bunge kutoa kabila kubwa la Albania, Talat Xhaferi, kwa kiasi kikubwa kilimsukuma rais huyo kukubali upinzani kuunda serikali.

Kiongozi wa upinzani amesema baada ya kushinda vita 67 dhidi ya 120, amesema atajaribu kuunda serikali mpya kufikia mwisho wa mwezi huu.