SWEDEN-ECUADOR

Kiongozi wa Mashtaka nchini Sweden aachana na mashtaka dhidi ya Julian Assange

Julian Assange Mmiliki wa mtandao wa Wikileaks
Julian Assange Mmiliki wa mtandao wa Wikileaks REUTERS/Peter Nicholls

Mkuu wa mashtaka nchini Sweden ameamua kuachana na mashtaka ya ubakaji dhidi ya mwanzilishi wa mtandao wa uchunguzi wa Wikileaks, Julian Assange.

Matangazo ya kibiashara

Marianne Ny amesema amefikia uamuzi kwa sababu ameshindwa kumpa Assange taarifa ya maandishi kuhusu mashtaka yanayomkabili.

Assange mwenye umri wa maika 45, amekuwa akiishi katika Ubalozi wa Ecuador jijini London kuanzia mwaka 2012.

Wakili wake, Per Samuelson, amesema uamuzi huo wa kiongozi wa mashtaka ni ushindi mkubwa kwa Assange.

Raia huyo wa Australia amekuwa akisema hawezi kwenda nchini Sweden kwa sababu ana hofu kuwa atasafirishwa kwa nguvu kwenda nchini Marekani, anakotuhumiwa kuvujisha siri za serikali.

Hata hivyo, Polisi jijini London wanasema watamkamata Assange ikiwa ataondoka katika Ubalozi huo.