UINGEREZA_USALAMA-MAUAJI

Mlipuko waua watu zaidi ya 19 baada ya tamasha mjini Manchester

Watu wawili wakikaa chini karibu ya barabara jirani ya ukumbi wa tamasha ya mwanamuziki Ariana Grande, Jumatatu usku Mei 23, 2017.
Watu wawili wakikaa chini karibu ya barabara jirani ya ukumbi wa tamasha ya mwanamuziki Ariana Grande, Jumatatu usku Mei 23, 2017. REUTERS/Andrew Yates

Watu 19 waliuawa usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne hii Mei 23 katika mlipuko uliotokea Manchester Arena, baada ya tamasha la mwanamuziki kutoka Marekani Ariana Grande.

Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa polisi inabaini tukio hilo kama "shambulio la kigaidi"." Kwa upande wake, Waziri wa Mkuu Theresa May, haraka ameshutumu "shambulio lenye kutisha la kigaidi."

Polisi katika mji wa Manchester imethibitisha kwamba mlipuko huo ulitokea saa 22: 30 usiku, saa za Uingereza, baada ya tamasha la nyota wa mitindo ya Pop kutoka Marekani Ariana Grande, mwanamuziki maarufu kwa vijana, katika mji wa Manchester Arena. Tamasha hilo liliendeshwa katika ukumbi wenye uwezo wa kuwapokea watu 21,000 ambapo kulikuwa walikua walikusanyika familia mbalimbali na watoto wadogo.

Mashahidi wa kwanza, ikiwa ni pamoja na jamaa walikua kusubiri watoto wao baada ya tamasha hilo kumalizika, wanasema walisikia mlipuko mmoja au milipuko miwili mikubwa katika eneo hilo wakati watu walikuwa kutoka nje ya ukumbi. Magari mengi ya wagonjwa yalielekea eneo la tukio, amearifu mwandishi wetu katika mji wa London, Muriel Delcroix. Taarifa kutoka polisi ya usalama wa barabarani ilisema mlipuko ulitokea katika ukumbi kulikoendeshwa tamasha. Eneo hili ni nafasi ya umma ambayo inaunganisha ukumbi huo na kituo cha treni karibu na Victoria kituo ambapo hupita treni za kawaida na treni za mwendo kasi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na polisi, mlipuko huo umegharimu maisha ya watu 22 na zaidi ya 50 waliojeruhiwa.Tukio ambalo vikosi vya usalama vinadai kwa sasa kama ni kitendo cha "kigaidi".

Ikiwa itathibitishwa kuwa ni shambulio la kigaidi, litakua mbaya zaidi kuwahi kukumba Uingereza tangu Julai mwaka 2005 wakati zaidi ya watu 50 walikufa kwenye misururu ya milipuko mjini London.

Eneo kulikotokea mulipuko limezingirwa na polisi waliojihami wanaendelea kushika doria.

Mwanamuziki Ariana Grande, pia, alisema saa chache baada ya mlipuko. Ariana Grand ameelezea masikitiko yake na kusem akua ameguswa na tukio hilo lililogharimu maisha ya watu 22.

Waziri Mkuu Theresa May anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama baadaye leo Jumanne.

Polisi ya Manchester wametenga eneo la usalama kote Manchester Arena ambako liliendeshwa tamasha la mwanamuziki Ariana Grande, Mei 22, 2017.
Polisi ya Manchester wametenga eneo la usalama kote Manchester Arena ambako liliendeshwa tamasha la mwanamuziki Ariana Grande, Mei 22, 2017. REUTERS/Jon Super