MAREKANI-UBELGIJI-NATO

Mapambano dhidi ya ugaidi kutawala mkutano mdogo wa NATO Brussels

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg Mei,24 2017, Brussels.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg Mei,24 2017, Brussels. REUTERS/Hannibal Hanschke

Mkutano wa muungano wa nchi za kujihami za Magharibii ulikua unasubiriwa na viongozi wengi wa nchi wanachama wa muungano huo. Siku ya Alhamisi, Mei 25, rais wa Marekani Donald Trump alikutana kwa mara ya kwanza na wenzake kutoka nchi wanachama wa NATO mjini Brussels.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani, ambaye alikosoa utendaji kazi wa muungano huo, alijaribu kuelekeza vipaumbele vyake. Katika kikao hicho kilichodumu saa tatu, viongozi kutoka nchini 28, kabla ya mada zote, walizungumzia kuhusu ulinzi wa kijeshi na mapambano dhidi ya ugaidi. Kabla ya kuhitimisha mkutano huo, Katibu Mkuu wa NATO, katika mkutano na waandishi wa habari, alizungumzia mada zilizogubika mazungumzo ya viongozi hao.

 NATO inakuwa mwanachama kamili dhidi ya kundi la Islamic State. Mbali na ishara kubwa ya kisiasa, hatuia inayofuata ni kuongeza ndege ya ukaguzi za AWACS pamoja na kutoa mafunzo kwa jeshi la Iraq. Lakini Jens Stoltenberg alisisitiza kuwa "kujiunga na muungano hatafsiri kwamba NATO itashiriki katika opereseni za kupambana dhidi ya kundi hili."

Kupeana taarifa kuhusu mitandao ya kigaidi kutaimarishwa. Kwa jambo hilo NATO itaweka kitengo maalum cha kujitolea kwa ajili hiyo.

Kuhusu matumizi ya kijeshi, suala ambalo Rais Trump amekua akifutilia mbali, viongozi wa nchi 28 walikubaliana kuhusu kuwekwa kwa ripoti za mwaka za kitaifa zitakazojumuisha sehemu tatu.

"Kwa maana gani nchi inaweza kufikia kuwekeza 2% ya Pato la Taifa katika ulinzi? Jinsi gani ya kuwekeza fedha za ziada ili kuongeza uwezo tunaohitaji? Na jinsi gani washirika watachangia katika shughuli mbalimbali, za NATO?".

Jens Stoltenberg alisema kuridhiswa na mkutano huo akisem akuwa NATO imefaidika mengi katikka mkutano huo. Kinachohitajika ni kuheshimu lengo la mkutano huu mdogo: kutuma ujumbe wa umoja kwa ulimwengu, alisema Bw Stoltenberg.