Mkutano wa G7 kufunguliwa, masuala nyeti kugubika mazungumzo

Polisi wa Italia wakipiga doria katika mitaa ya Taormina, Mei 18,2017.
Polisi wa Italia wakipiga doria katika mitaa ya Taormina, Mei 18,2017. REUTERS/Antonio Parrinello

Ijumaa hii Mei 26, mkutano wa 43 wa nchi zilizostawi kiuchumi G7 unaanza katika mji wa Taormina, Sicily (Italia). Mkutano ambao unaweza kuwa usio wa kawaida mwaka huu kutokana hasa na kuwepo kwa marais wengi wapya, ambao hawajawahi kushiriki mkutano huu.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, lakini pia rais wa Marekani Donald Trump au Theresa Mei, Waziri Mkuu wa Uingereza. Hadi Jumamosi marais wa Ufaransa, Marekani, China, Japan, Ujerumani, Uingereza na Italia watajadili masuala tofauti: uhusiano wa kimataifa, usalama, uchumi wa dunia, uvumbuzi na maendeleo katika Afrika na pia hali ya hewa, mada ambayo inaweza kutawala mkutano huu wa siku mbili.

 

Ni mkutano usio kuwa wa kawaida wa nchi zilizostawi kiuchumi ambao unazinduliwa leo Ijumaa, katika mji wa Taormina. Kama inavyothibitishwa na chanzo kutoka Elysee, ripoti ya mwisho imeanza kusikika kabla ya ufunguzi wa mkutano wa G7 mwaka huu.

Marekani imeendelea kulaumiwa kuhusu mada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya ongezeko la joto duniani. Rais wa Marekani alitangaza kuwa atasitisha baada ya mkutano huo, uwezekano wa Marekani kuondoka kwenye makubaliano ya Paris.

Viongozi mbalimbali katika mkutano huo watajaribu kushawishi msimamo wa Marekani ambayo inapinga suala la kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. kazi ambayo tayari walianza viongozi wa Ulaya Alhamisi hi mjini Brussels katika mkutano wa muungano wa kujihami wa nchi za Magharibi (NATO).

Jambo lingine nyeti: uchumi wa dunia. Kwa mara nyingine tena msimamo wa Marekani kutaka kulinda uchumi wake tangu kuwasili madarakani kwa Donald Trump, jambo ambalo linapingwa na viongozi wengine ambao wanataka udhibiti mzuri wa biashara duniani.

Hatimaye, usalama na kupambana na ugaidi bila shaka ni miongoni mwa mada nyeti zitakazojadiliwa katika mkutano huu wa Taormina.