FILAMU

Mshindi wa tamasha la Filamu maarufu kama Cannes kufahamika mwishoni mwa wiki

Baadhi ya wadau wa Filamu nchini Ufaransa
Baadhi ya wadau wa Filamu nchini Ufaransa 路透社

Makala ya 70 ya tamasha la kila mwaka la Filamu maarufu kama Cannes Film Festival, linamalizika siku ya Jumapili mjini Cannes nchini Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Tangu kuzinduliwa kwa tamasha hili mwaka 1946, kila mwaka watunzi, wasimamizi na waigizaji wa Filamu mbalimbali huwasilisha filamu zao kila mwezi wa Mei kutoka kote duniani zinazoshindanishwa na mshindi kupatikana.

Aidha, watalaam wa filamu huwa wanabadilishana uzoezfu na kujadiliana namna ya kuboresha sekta hiyo duniani ambayo imetoa ajira nyingi kwa watu.

Mwaka 2017, filamu 19 kutoka maeneo mbalimbali duniani zinashindanishwa kushinda tuzo ya kila mwaka inayofahamika kama Palme d'Or.

Mojawapo ya filamu inayopewa nafasi kubwa ni "I Am Not A Witch" ikimaanisha kuwa mimi sio mchawi, inaongozwa na Rungano Nyoni raia wa Uingereza mwenye asili ya Zambia.

Filamu hii inazungumzia kuhusu imani za kishirikiana barani Afrika na ilivyo hatari kuishi katika mazingira hayo ikiwa mtu ataaminiwa kuhusika.