UINGEREZA-IS SHAMBULIO-USALAMA

IS yadai kuhusika na shambulio la London

Kikosi cha polisi kikiendesha uchunguzi wake kwenye daraja la London Jumapili hii, Juni 4,2016.
Kikosi cha polisi kikiendesha uchunguzi wake kwenye daraja la London Jumapili hii, Juni 4,2016. REUTERS/Neil Hall

Polisi ya Uingereza imeendelea na msako hadi usiku wa manane katika eneo maarufu la Barking mashaiki mwa mji wa London, ambapo watu kadhaa walikamatwa. Kundi la Islamic State lilikiri siku ya Jumap[ili kwamba lilihusika na shambulio hilo.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa mpya, mkuu wakikosi cha kukabiliana na ugaidi alisema kwamba wachunguzi wamekua wakiendelea na kazi yao na wametambua watu walilioendesha shambulio dhidi ya mji wa London siku ya Jumamosi usiku.

Polisi kwa sasa inachunguza kama watu hao walipata msaada wowote kutoka watu wengine kwa kuandaa shambulio hili. Vikosi vya usalama waliendesha mfululizo wa mashambulizi katika eneo la Barking, mashariki mwa London mapema Jumapili asubuhi.

Watu kumi na mbili ikiwa ni pamoja na wanawake wanne walikamatwa wakituhumiwa kuhusika katika shambulio hilo.

Katika shambulio hilo watu saba waliuawa na wengine hamsini walijeruhiwa .

Wachunguzi wanajaribu kubaini ikiwa wanaume watatu walioendesha basi lao dogo na kuwagonga wapita njia kabla ya kuwachoma visu wengine wengi walipata msaada wowote.

Watu kumi na mbili wanashikiliwa kufuatia msako wa polisi mashariki mwa London.

Kundi la Islamic State lilisema siku ya Jumapili lwamba lilihusika na shambulio hilo.
Raia mmoja kutoka Ufaransa aliyeuawa ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulio hilo

Wakati huo huo katika mji wa London, polisi imeeleza kwamba maeneo ya usalama yaliotengwa katika mitaa iliyolengwa na mashambulizi yatasalia chini ya ulinzi mkali kwa muda fulani, na hatua za usalama katika mji mkuu wa Uingereza zitajadiliwa upya.