UINGEREZA-EU

EU iko tayari kuanza majadiliano kuhusu Kujiondoa kwa Uingereza

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema haoni kikwazo cha kuanza kwa majadiliano ya Uingereza kujitenga na Umoja wa Ulaya kama yalivyopangwa baada ya waziri mkuu wa Uingereza kushindwa kura za wengi katika uchaguzi wa alhamisi.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel
Matangazo ya kibiashara

Kansela wa ujerumani anaamini Uingereza itazingatia ratiba akiongeza kuwa Umoja wa ulaya uko tayari na hivyo Uingereza itaendelea kuwa mshirika mzuri kufuatia majadiliano yanayotaraji kuanza June 19.

Hii ni kauli yake ya kwanza tangu chama cha waziri mkuu wa Uingereza Conservative kupoteza viti 13 katika uchaguzi uliofanyika nchini Uingereza siku ya alhamisi.

Matokeo hayo yamekiacha chama cha Bi May na wabunge 8 katika bunge ambapo waziri mkuu huyo aliitish auchaguzi mdogo ili kujihakikishia ndoto yake ya kujitenga na Moja wa Ulaya.

Hata hivyo Theresa May baada ya kuonana na malkia Elizabeth wa 2, alisema chama chake cha Conservative ndio chenye uhalali wa kuunda Serikali na kwamba ataiongoza nchi yake kujiondoa kwenye umoja wa Ulaya.