UFARANSA-UCHAGUZI

Wafaransa wapiga kura za ubunge hii leo

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron REUTERS/Stephane Mahe

Wapiga kura nchini Ufaransa hii leo wanapiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge huku chama Rais Emmanuel Macron kikionekana kujipanga vizuri kupata idadi kubwa ya wabunge.

Matangazo ya kibiashara

Macron ameanza vizuri katika majuma matano ya mwanzo tangu mashinde mpinzani wake katika kinyang’anyiro cha urais bi Marine Le Pen na kuwa rais mwenye umri mdogo kuwahi kuongoza Ufaransa, akitaja baraza la mawaziri lililovuka mipaka ya mrengo wa kulia na kushoto jambo lililovuta hisia kubwa katika mikutano ya kimataifa.

Chama chake cha Republique en Marche ambacho alikianzisha mwezi Aprili 2016 kama jukwaa kwa ajili ya jitihada zake za kuwania urais, sasa kinahitaji idadi kubwa ya waliowengi bungeni kwa ajili yake kushinikiza kupitisha marekebisho aliyoahidi.

Kura za maoni zinaonyesha kuwa chama cha Macron kinaweza kuchukua hadi asilimia 30 ya kura katika mzunguko wa kwanza kesho Jumapili, ambazo zitakiweka katika nafasi nzuri ya kupata idadi kubwa ya wabunge katika mzunguko wa pili baada ya juma moja.