UINGEREZA-USALAMA

Moto mkubwa wateketeza jengo la Grenfell Tower London

Jengo refu mjini London la Grenfell Tower lazidiwa na moto.
Jengo refu mjini London la Grenfell Tower lazidiwa na moto. REUTERS/Toby Melville

Moto mkubwa umeteketeza jengo refu la makazi la Grenfell Tower katika barabara ya Latimer, magharibi mwa jiji la London. Mashahidi wanasema kuwa baadhi ya watu bado wamekwama ndani ya jengo hilo linalo waka moto.

Matangazo ya kibiashara

Watu walio shuhudia tukio hilo wanasema, moto huo umeleta mshituko mkubwa katika mji wa London, hali ambayo iliyosababisha baadhi ya watu kushindwa kutoka katika nyumba zao.

Moto huo bado unaendelea kuwaka na kuunguza jengo hilo, hukuvikosi vya uokoaji na zima moto takriban 200 vikiendelea na kazi hiyo.

Inaarifiwa kuwa moto huo ulianza saa 01:16, saa za Uingereza laikini vikosi vya uokoaji vinaendelea kukabiliana na moto huo.

Maafisa wa usalama wamebaini kwamba watu wawili tu ndio wamebainika kuwa wameathirika na moshi wa moto huo na wnaendelea kupata matibabu.

Uingereza imeendelea kukumbwa na majanga mbalimbali ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa.