UJERUMANI

Kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Kohl afariki dunia

Aliyekuwa Kansela wa Ujerumani Helmut Kohl
Aliyekuwa Kansela wa Ujerumani Helmut Kohl REUTERS/Johannes Eisele/File Photo

Aliyekuwa Kansela wa Ujerumani Helmut Kohl amefariki dunia.

Matangazo ya kibiashara

Kohl aliongoza nchi hiyo ya bara Ulaya kati ya mwaka 1982-1998.

Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87.

Atakumbukwa kama kiongozi aliyeongoza Ujerumani katika kipindi kigumu cha mgawanyiko wa nchi yake na kufanikiwa kuiunganisha mwaka 1989 baada ya kuangushwa kwa ukuta wa Berlin.

Mkuu wa Tume wa Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker amesema Kohl atakumbukwa sana kwa juhudi zake za kuanzisha na kufanikisha Umoja wa Ulaya na matumizi ya sarafu ya Euro.

Mwenyekiti huyo wa zamani wa chama tawala nchini Ujerumani cha Christian Democratic Union amekumbukwa pia na rais wa zamani wa Marekani George H.W. Bush kama kiongozi shupavu.