UINGEREZA-MOTO

Polisi nchini Uingereza wasema walioangamia katika jengo lililowaka moto hawatambuliwa wote

Polisi jijini London wakilinda usalama
Polisi jijini London wakilinda usalama Reuters/Neil Hall

Polisi nchini Uingereza wanaonya kuwa itakuwa ni vigumu kuwatambua watu wote walioangamia katika jengo lililotetekea kwa moto mapema wiki hii jijini London.

Matangazo ya kibiashara

Hadi sasa watu 17 wamethibitishwa kupoteza maisha huku ikihofiwa kuwa huenda idadi ikaongezeka na kufikia 60.

Maafisa wa uokoaji wamekuwa wakiendelea kutafuta miili ya watu wanaominiwa walikwama ndani ya jengo hilo.

Watalaam wa kuzima moto wanasema hawatarajii kuwapata manusura zaidi wa mkasa huo.

Waziri Mkuu Theresa May alitembelea eneo hilo na kuagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina. Chanzo cha moto huo hakijafahamika. Soma hii pia.Bonyeza

Hata hivyo, amekosolewa kwa kushindwa kuonana na waathiriwa wa mkasa huo.

Haijabainika chanzo cha moto huo mkubwa ambao haujawahi kuonekana katika miaka ya hivi karibuni nchini humo.

Mkasa huu umesababisha ucheleweshwaji wa kuundwa kwa serikali mpya baada ya uchaguzi wiki iliyopita.