UFARANSA-UCHAGUZI

Uchaguzi wa wabunge Ufaransa wafanyika jumapili

Raisi wa Ufaransa Emmanuel Macron
Raisi wa Ufaransa Emmanuel Macron REUTERS/Matthieu Alexandre/Pool

Wapiga kura nchini Ufaransa wanachagua wabunge leo jumapili,uchaguzi unaotazamiwa kukipa ushindi mkubwa chama kichanga cha raisi Emanuel Macron ambaye atakamilisha mpango wake wa kufanya mageuzi katika siasa za taifa.

Matangazo ya kibiashara

Bunge jipya linataraji kushuhudia mageuzi ya uwepo wa kizazi kipya cha wabunge vijana zaidi,wa kike na wenye mitazamo na makabila mbalimbali wakishinda viti kufuatia muamko uliosababishwa na ushindi wa Macron katika uchaguzi mkuu uliopita.

Vyama vingine vimewaasa wapigakura kuwaunga mkono mahasimu wa Macron ili kuepusha mamlaka yote kwenda kwa chama kimoja cha Macron pekee.

Chama cha raisi Macron kiliundwa miezi 15 tu iliyopita na nusu ya wagombea wake wana uzoefu na wengine hawana kabisa uzoefu wa kisiasa.

Chama kinahitaji viti mia mbili themanini na tisa ili kuongoza bunge la kitaifa lenye jumla ya wabunge 577 ambapo sasa chama cha LREM kinatazamiwa kupata zaidi ya viti 400.