UINGEREZA-UGAIDI

Waziri Mkuu May: Shambulizi jijini London liliwalenga Waislamu

Shambulizi dhidi ya Waislamu Kaskazini mwa jiji la London
Shambulizi dhidi ya Waislamu Kaskazini mwa jiji la London REUTERS/James Cropper

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May anasema shambulizi la kigaidi nje ya msikiti Kaskazini mwa jiji London, linasikitisha na kuchosha.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo limesababisha kifo cha mtu mmoja na zaidi ya 10 kujeruhiwa.

Waliojeruhiwa wanaendelea kupata matibabu hospitalini.

Bi. May amesema kuwa shambulizi hilo liliwalenga Waislamu.

Kongozi huyo wa serikali ameongoza kikao cha usalama mapema siku ya Jumatatu na kusisitiza kuwa, Uingereza haitavumilia ugaidi na mafunzo ya kijihadi.

Ni tukio lililotokea wakati huu waumini wa dini hiyo wakiendelea kuwa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Polisi wamesema watu wote waliojeruhiwa na aliyepoteza maisha, wote ni Waislamu.

Dereva wa basi liliwagonga Waislamu hao, amekamatwa na Polisi wanasema wanaamini alitekeza shambulizi hilo peke yake.

Uingereza hivi karibuni imeendelea kushuhudia matukio ya kigaidi.