UFARANSA-IRAQ-VYOMBO VYA HABARI

Mwanahabari Stephan Villeneuve auawa katika mlipuko Mosul

Askari wa bataliani ya 9 ya vikosi vya kivita nchini Iraq katika moja ya mitaa ya Mosul Magharibi, Juni 19, 2017.
Askari wa bataliani ya 9 ya vikosi vya kivita nchini Iraq katika moja ya mitaa ya Mosul Magharibi, Juni 19, 2017. REUTERS/Alkis Konstantinidis

Mwanahabari kutoka Ufaransa Stephan Villeneuve, ambae alikua akifanya uchunguzi kwa niaba ya kituo cha France 2 katika makala ya "Evoye special", amefariki kutokana na majeraha alioyapata baada ya kulipuka kwa bomu la kutegwa ardhini lililolipuka siku ya Jumatatu mjini Mosul.

Matangazo ya kibiashara

Wanahabari wengine wawili kutoka Ufaransa walijeruhiwa, huku mkalimani wao kutoka Iraq akipoteza maisha katika mlipuko huo.

Jumanne hii Juni 20 kituo cha France Télévision kimetangaza taarifa ya kifo cha mmoja wa wanahabari wake kufuatia kulipuka kwa bomu la kutegwa ardhini katika mji wa Mosul. Stéphan Villeneuve, ambae alikua akiandaa makala ya "Envoyé spécial" ya kituo cha France 2 akishirikiana na Véronique Robert, amefariki kutokana na maeraha alioyapata.

"Uongozi wa kituo cha France Télévisions kinatoa rambirambi zake kwa familia ya mwanahabari huyo, ambaye ameacha mkee na watoto wanne, " imeeleza taarifa ya uongozi wa mawasiliano wa kito cha France Televisions, taarifa ambayo ilitumwa kwenye ofisi ya shirika la habari la AFP usiku wa kuamkia leo Jumanne.

Mwenzake, Véronique Robert, amejeruhiwa vibaya. Walikua wakiongozana na samuel Forey, mwandishi wa habari wa vituo kadhaa vya habari nchini Iraq, ambaye pia alifariki katika mlipuko huo,Nicolas Delesalle, ripota wa kituo cha Telerama, ameandika kwenye Twitter
Mkalimani wa waandishi hao watatu, Bakhtiyar Haddad, alifariki papo hapo. Alikua rafiki wa wanahabari wengi kutoka Ufaransa na alishirikiana na wanahabari wengi wa RFI. Alikua akiambatana na wanahabari wengi katika maeneo hatari.